Watu wengi huamini kwamba kwa kuhudhuria kanisani tu, wanakuwa watu wa kweli wa Mungu.
Walakini, kwa sheria ya Mungu ya uzima, Anatofautisha kati ya watu wa kweli na wa uongo.
Watu wa kweli wa Mungu, ambao wana uraia wa mbinguni, lazima waishike siku ya Sabato, ambayo ni ukumbusho wa uweza wa Muumba, na Pasaka, ambayo ni ukumbusho wa uweza wa Mkombozi.
Kama vile Solomoni, mfalme wa hekima, alivyotumia nyuki na vipepeo kutofautisha ua jipya na ua bandia, Mungu hutofautisha watu Wake wa kweli kupitia amri Zake kama siku ya Sabato na Pasaka.
Leo, waumini wengi sana ulimwenguni kote wanazishika amri za Mungu—ishara ya watu wa Mungu—waliorudishwa kupitia mafundisho ya Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama.
Kwa maana, kama nilivyokwisha kuwaambia mara nyingi kabla, nami sasa nasema tena hata kwa machozi, watu wengi wanaishi kama adui wa msalaba wa Kristo.
Mwisho wa watu hao ni maangamizi, Mungu wao ni tumbo, na utukufu wao ni aibu, na mawazo yao yamo katika mambo ya dunia.
Lakini uraia wetu uko mbinguni. . . .
Wafilipi 3:18–20
“ ‘Mtaishika Sabato, kwa sababu ni takatifu kwenu. Yeyote atakayeinajisi lazima auawe, yeyote atakayefanya kazi siku hiyo lazima akafie mbali na watu wake.
Kutoka 31:14
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha