Wale wanaomwamini Mungu lazima waiadhimishe Sikukuu ya Vibanda kulingana na mafundisho ya Mungu. Hii ni kwa sababu Mungu Alisema kupitia nabii Zekaria kwamba Atawapa Roho Mtakatifu wale wanaoadhimisha Sikukuu ya Vibanda na kuleta adhabu juu ya wale ambao hawaiadhimishi.
Wakati wa ujio Wake wa kwanza, Yesu Alitoa Roho Mtakatifu; wakati wa ujio Wake wa pili, Roho na Bibi arusi Wanatoa Roho Mtakatifu katika Sikukuu ya Vibanda. Unabii wa Biblia, “Roho na Bibi arusi Watatoa maji ya uzima,” “Maji yaliyo hai yatatoka Yerusalemu,” na “Mto wa maji ya uzima unatiririka kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu” unatabiri kwamba Yerusalemu Mama wa Mbinguni Atatoa Roho Mtakatifu na mafundisho yanayoongoza kwenye uzima.
Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia... Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Yesu akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema . . . Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yanavyosema, vijito vya maji ya uzima vitatiririka kutoka ndani yake.” Yesu aliposema haya, alimaanisha Roho Mtakatifu, ambaye wote waliomwamini wangempokea . . . Yohana 7:2–39
Roho na bibi arusi wanasema, “Njoo!” Naye asikiaye na aseme, “Njoo!” Yeyote mwenye kiu na aje, na kila anayetaka na anywe maji ya uzima bure. Ufunuo 22:17
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha