Ufalme wao ulipozidi kuwa na nguvu, wafalme kama Rehoboamu, Sauli, Uzia, Ahazi, na Sedekia walijiinua na kuwa na kiburi.
Hatimaye, walitenda dhambi dhidi ya Mungu nao wakaangamizwa.
Kwa upande mwingine, Yothamu, Daudi, Danieli, na marafiki zake watatu walikuwa waaminifu kwa Mungu sikuzote nao walibarikiwa na Mungu.
Hili ni somo muhimu linaloonyesha mwelekeo wa imani ambao waumini wa Kanisa la Mungu wanapaswa kufuata leo.
Wanapaswa kuwa waaminifu kwa Mungu sikuzote, si kwa imani inayoyumba kutegemea mazingira na hali.
Pia, wanapaswa kuamini katika msaada wa Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama na kutekeleza kazi ya injili kulingana na neno la Mungu.
Ndipo, Mungu Atakapoifanya Sayuni kuwa yenye nguvu, mafanikio, na bora juu ya ulimwengu mzima kama ufalme wa Daudi.
Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa Bwana. Hakulishika neno la Bwana, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi, hakumuuliza Bwana.
Kwa hiyo Bwana alimuua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese.
1 Nyakati 10:13–14
Yothamu akaendelea kuwa na nguvu kwa sababu alienenda kwa ukamilifu mbele za Bwana Mungu wake.
2 Nyakati 27:6
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha