Mungu Aliteua siku ya kwanza ya mwezi wa saba wa kalenda takatifu kama Sikukuu ya Tarumbeta ili kwamba tukumbuke Siku ya Upatanisho, tukikumbuka wakati Aliposamehe dhambi za Waisraeli ambao walikuwa wameanguka katika ibada ya sanamu na Kuwapa seti ya pili ya Amri Kumi. Zaidi ya hayo, kama vile tarumbeta zilivyopigwa kwenye Sikukuu ya Tarumbeta ili kuitaka toba, Yesu pia Alikuja duniani na Kuwahimiza wanadamu watubu, Akisema, “Tubuni.”
Kama tunavyoweza kuona katika Mfano wa Mwana Mpotevu na katika simulizi ya Yona kuwaongoza watu 120,000 huko Ninawi kwenye wokovu, baraka kuu kutoka kwa Mungu huandaliwa sikuzote kufuatia kazi ya toba. Leo pia, lazima tufikie toba kamili—kama Yona—kwa ajili ya macho na mioyo tuliyoigeuza kuelekea ulimwengu, na tupige tarumbeta, tukiita ulimwengu wote kuwarudia Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama.
“Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na siku ya mapumziko, kusanyiko takatifu la ukumbusho litakaloadhimishwa kwa kupiga tarumbeta.
“Kwa hiyo, ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asema BWANA Mwenyezi. Tubuni! Geukeni kutoka makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu.”
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha