Kinabii Biblia inafafanua nyakati hizi kama wakati wa mgogoro mkubwa.
Vita vinapopamba moto kati ya mataifa na maafa mengi ya hali ya hewa yanayotokea, watu wanapanga mipango ya kukimbilia angani, vilindi vya bahari, au chini ya ardhi.
Walakini, Biblia inasema kwamba hakuna kimbilio la wokovu isipokuwa Sayuni, mahali anapokaa Mungu Mama.
Kama vile Mungu Alivyomfunulia na kufasiri ndoto ya Mfalme Nebukadneza kwa Danieli, leo Amefunua kwamba kimbilio salama zaidi katikati ya maafa ni Mungu Mama.
Kama vile watoto wanavyohisi usalama zaidi mikononi mwa mama yao wakati wa hatari, Mungu Amefunua kwamba Mungu Mama ni mahali salama zaidi kwa wanadamu katika maafa.
BWANA asema, “Nitafagia kila kitu kutoka kwenye uso wa dunia.”
“Nitafagilia mbali watu na wanyama; nitafagilia mbali ndege wa angani na samaki wa baharini. Wafanyao maovu watapata tu kokoto, nami nitamkatilia mbali mwanadamu atoke katika dunia,” asema BWANA.
Sefania 1:2–3
“Lakini kama huyo mtumishi ni mwovu, naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’
kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi.
Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua.
Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wanafiki, mahali ambako kutakuwa ni kulia na kusaga meno.”
Mathayo 24:48–51
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha