Ijapokuwa Yuda Iskariote alikuwa mwanafunzi wa Yesu, moyo wake ulizingatia utajiri wa kimwili badala ya ufalme wa mbinguni. Alijichukulia fedha kutoka kwenye mfuko aliokabidhiwa na hata akamkemea Maria kwa kutumia manukato ya gharama kubwa kumuandaa Yesu kwa ajili ya maziko yake. Kama vile historia ya Daudi na Ahithofeli ilivyotumika kama kivuli cha unabii, Yuda alimuuza Yesu kwa vipande thelathini vya fedha na hatimaye akatimiza unabii wa kifo chake mwenyewe kwa kujinyonga.
Kama vile Yuda Iskariote alivyojaribiwa na mfuko wa fedha aliokabidhiwa, sisi pia, lazima tuwe macho dhidi ya majaribu ya Shetani, ambayo mara nyingi hutokana na mazingira yetu ya karibu. Lazima tuishi imani yetu kwa maneno na matendo yenye neema. Wale wanaofuata kwa uaminifu njia ya kuelekea ufalme wa mbinguni inayoongozwa na Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama watamtukuza Mungu na kufurahia utukufu wa milele katika ufalme wa mbinguni.
Kwa kuwa hatukuja humu duniani na kitu chochote, wala hatuwezi kutoka humu na kitu. Kwa maana kupenda fedha ndiyo shina moja la maovu ya kila namna. Baadhi ya watu wakitamani fedha, wameiacha imani na kujichoma wenyewe kwa maumivu mengi. 1 Timotheo 6:7–10
Akawajibu, “Ni mmoja miongoni mwenu ninyi kumi na wawili, yule anayechovya mkate kwenye bakuli pamoja nami. Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu. Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa!” Markoo 14:20–21
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha