Katika wakati wa Mose, Mungu Aliwaokoa Waisraeli walioadhimisha Pasaka kutokana na pigo na Akaadhibu Familia zote za Misri ambazo hazikuadhimisha Pasaka. Hii inatuonyesha jinsi tunavyoweza kuokolewa kutokana na maafa na kupokea uzima wa milele katika enzi hii, pia.
Pasaka ya Agano Jipya ni siku ambayo wanadamu wanarithi mwili na damu ya Mungu na kutiwa muhuri kama watoto wa Mungu, na siku ambapo wanasamehewa dhambi zao walizotenda Mbinguni na kupokea uzima wa milele.
Hii ndiyo sababu Mungu hutupa nafasi moja zaidi kuadhimisha Pasaka kwenye siku ya 14 ya mwezi wa pili kwenye kalenda takatifu, Akitamani sana ulimwengu wote uadhimishe Pasaka na kupokea wokovu.
“Waambie Waisraeli: ‘ . . hata hivyo wanaweza kuadhimisha Pasaka ya BWANA. Wataiadhimisha wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Watamla mwana-kondoo, pamoja na mkate usiotiwa chachu, na mboga chungu. . . . asipoadhimisha Pasaka, mtu huyo hana budi kukatiliwa mbali na watu wake kwa sababu hakutoa sadaka ya BWANA kwa wakati ulioamriwa. Mtu huyo atawajibika kubeba matokeo ya dhambi yake.
Hesabu 9:10-13
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha