Kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, Mungu Alitupa Biblia na kuanzisha sheria ya agano jipya.
Kama vile Solomoni alivyoweza kuamua mama wa kweli wa huyo mtoto alikuwa nani kupitia silika ya upendo wa mama, katika enzi hii, Mungu Anawatambua wale wanaolishika agano jipya, ambalo Mungu Aliamuru, kama watoto Wake wateule, na Anawajalia baraka ya wokovu.
Leo, Kanisa la Mungu linafuata mwongozo wa Kristo Ahnsahnghong na Yerusalemu Mpya Mama wa Mbinguni. Walirudisha agano jipya ambalo lilikuwa limepotea, kama vile Sabato na Pasaka, na kutupatia mafundisho yote yanayohitajika kwa ajili ya wokovu wa roho zetu ambao ndio lengo la imani yetu. Hii ndiyo maana Kanisa la Mungu tu lina ahadi ya wokovu.
Hili ndilo asemalo BWANA: “Kwa dhambi tatu za Yuda, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA na hawakuzishika amri zake, kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo, miungu ambayo babu zao waliifuata. . . . Amosi 2:4
Ingawa hamjamwona, mnampenda; tena ingawa sasa hammwoni, mnamwamini na kujawa na furaha isiyoneneka yenye utukufu usioelezeka. Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu. 1 Petro 1:8–9
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha