Kama vile Adamu na Eva walivyotenda dhambi kwa sababu walisahau sheria ya Mungu, “Lazima usile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya,” kila tunaposahau sheria ya Mungu, tunatenda dhambi na kupokea maafa.
Hata katika enzi hii, Mungu Anasema kwamba maafa ya mwisho yatakuja kwa sababu ulimwengu umesahau sheria ya Mungu—siku ya Sabato na Pasaka ya agano jipya, na hauziadhimishi.
Wanadamu ni nafsi [malaika] waliotenda dhambi mbinguni na kutupwa chini duniani.
Wanaweza kurudi mbinguni pale tu wanapolitii neno la Mungu wakiwa wanaishi hapa duniani.
Kama vile Mfalme Hezekia alivyopokea baraka kwa kushika sheria [Pasaka] kulingana na neno la Mungu, Kanisa la Mungu linatii mapenzi ya Mungu kwa kushika sheria ya Mungu—agano jipya.
Jihadharini msimsahau BWANA Mungu wenu, mkashindwa kushika maagizo yake, sheria na amri zake ambazo ninawapa leo.
Kumbukumbu la Torati 8:11
“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo wachafu na kufanya miujiza mingi?’
. . . ‘Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’
Mathayo 7:21–23
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha