Yesu Aliwafundisha wanadamu kupitia Mfano wa Tajiri na Lazaro kwamba maisha katika dunia hii sio mwisho. Lazaro, ingawa alikuwa maskini duniani, aliishi kama msafiri akiwa na tumaini la mbinguni na hatimaye akapata furaha.
Kwa upande mwingine, yule tajiri aliishi maisha ya anasa, lakini aliishi kama anayetangatanga.
Alishindwa kujiandaa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni na hatimaye akateseka jehanamu.
Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama Waliwapa wanadamu ushuhuda wa mababa wa imani kama vile Abrahamu na Mose waliosema, “Sisi ni wageni na wasafiri katika dunia hii.”
Kupitia rekodi hizi katika Biblia, Waliwaelimisha wanadamu wote kwamba nyumbani kwao pa kweli ambapo lazima warudi ni ufalme wa mbinguni.
Watu hawa wote wakafa katika imani bila kuzipokea zile ahadi, lakini waliziona kwa mbali na kuzishangilia. Nao walikubali kwamba walikuwa wageni na wasiokuwa na maskani hapa duniani.
Waebrania 11:13
Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini Mungu, niaminini na mimi pia.
Nyumbani kwa Baba yangu kuna makao mengi. . . . Naenda kuwaandalia makao. . . .
ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo.”
Yohana 14:1–3
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha