Katika enzi ya Roho Mtakatifu, Mungu Alitabiri katika Biblia kwamba kutakuwa na vita vikuu vya kiroho kati ya huyo Mwanamke na watoto Wake waliosalia na Shetani na wafuasi wake. Mungu Anapowatenganisha wale watakaookolewa na wale ambao hawataokolewa, kwa kusimama tu kwenye upande wa huyo Mwanamke, ambaye ni Mungu Mama, tunaweza kushinda vile vita vikuu vya kiroho na kupokea baraka ya wokovu.
Mungu Ahnsahnghong Alitujulisha wazi kwamba Mungu Mama yupo kupitia mfumo wa familia ya duniani na mchakato wa kuumbwa kwa Eva na kwamba waumini wa Kanisa la Mungu, yaani, watoto waliosalia wa huyo Mwanamke, wanapaswa kuhubiri utukufu wa Yerusalemu Mama kwa ulimwengu.
Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke na likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari. . . . Ufunuo 12:17–13:1
Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu, hawatanyamaza mchana wala usiku. Ninyi wenye kumwita BWANA, msitulie, msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemu na kuufanya uwe sifa ya dunia. Isaya 62:6–7
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha