Mungu Aliwaumba wale walio na uraia mbinguni wenye mioyo inayothamini Sabato, Pasaka na sikukuu saba katika nyakati tatu ili kwamba washike sheria Zake. Kwa hiyo, kwa wote wamwitao Mungu kwa midomo yao lakini wanafuata sheria ya mungu jua badala ya sheria ya Mungu, Anawapa onyo kuhusu dhambi yao, kwa kusema: “Sikuwajua ninyi.”
Hata kama ulimwengu wote unabadilika, kitu kimoja ambacho hakibadiliki kamwe ni sheria ya Mungu. Yesu Aliadhimisha Pasaka miaka 2,000 iliyopita, na Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama pia Wameiadhimisha katika enzi ya Roho Mtakatifu. Kufuata mfano Wao kwa kuadhimisha Pasaka ndiyo imani sahihi, inayomlenga Mungu.
“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Ndipo nitakapowaambia wazi, ‘Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’ Mathayo 7:21–23
Lakini mtu aliyetakasika na hayuko safarini asipoiadhimisha Pasaka, mtu huyo hana budi kukatiliwa mbali na watu wake . . . Mtu huyo atawajibika kubeba matokeo ya dhambi yake. Hesabu 9:13
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha