Kama ilivyoandikwa, “[Y]eyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Kristo Yesu atateswa,” na kama Yesu Alivyosema, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima . . . auchukue msalaba wake, anifuate,” mateso ya muda mfupi lazima yafuate maisha ya wale wote wanaoishi kwa ajili ya utukufu wa ufalme wa mbinguni.
Esau na Yuda Iskariote waliishi kulingana na mwili, wakifuatia anasa za dhambi, na hatimaye wakapoteza baraka za ufalme wa mbinguni. Walakini, Mose, Yakobo, Danieli, na marafiki zake watatu walishinda magumu kwa kuthamini raha za mbinguni zaidi. Vivyo hivyo, waumini wa Kanisa la Mungu huweka tumaini lao katika raha za mbinguni zilizoahidiwa na Mungu, wakijitoa wenyewe kuhubiri baraka za siku ya Sabato na Pasaka ya agano jipya, kama vile Alivyoamuru.
Kwa imani, Mose alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao. Akachagua kupata mateso pamoja na watu wa Mungu, kuliko kujifurahisha kwa anasa za dhambi kwa kitambo kidogo tu. Aliona kushutumiwa kwa ajili ya Kristo ni utajiri mkubwa kuliko hazina za Misri, maana alikuwa anatazamia kupata thawabu baadaye. Waebrania 11:24–26
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha