Noa aliamini katika baraka za Mungu ingawa alikabili upweke alipokuwa akijenga safina kwa muda mrefu. Mose alipendelea kuteseka pamoja na watu wa Mungu badala ya kufurahia utukufu wake kama mwana-mfalme katika Misri. Mtume Paulo alishangilia katika nafasi ya kutoa ufalme wa mbinguni kwa watu, licha ya kukabili magumu mengi. Vivyo hivyo, waumini wa Kanisa la Mungu wanatembea njia ya imani kwa furaha, wakiichukua misalaba yao.
Sikuzote Mama wa Mbinguni Anatukumbusha, “Je, hatuna tumaini la ufalme wa mbinguni?” Kwa hiyo, iwe ni watakatifu au wachungaji watendakazi wanaofanya kazi katika mstari wa mbele, kila mtu anapaswa kuangalia baraka za ufalme wa mbinguni zilizoandaliwa zaidi ya vikwazo vinavyojitokeza mbele ya macho yetu tunapoichukua misalaba yetu wenyewe.
Aliona kushutumiwa kwa ajili ya Kristo ni utajiri mkubwa zaidi kuliko hazina za Misri, maana alikuwa anatazamia kupata thawabu baadaye. Waebrania 11:26
kwa maana mkiishi kwa kuufuata mwili, mtakufa, lakini kama mkiyaua matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio watoto wa Mungu. . . . naam, tukiteswa pamoja naye tupate pia kutukuzwa pamoja naye. Nayahesabu mateso yetu ya wakati huu kuwa si kitu kulinganisha na utukufu utakaodhihirishwa kwetu. Warumi 8:13–18
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha