Mafanikio au kushindwa kwa kazi ya injili kunategemea jinsi imani yetu katika Mungu ilivyo imara. Kama vile Mungu Alivyotuonyesha katika vita katika siku za Gideoni na Yoshua, wale ambao imani yao inatikiswa na mazingira na hali zao wanatengwa na jeshi la Mungu, na wale tu wenye imani thabiti katika Mungu ndio hutumiwa kuandika historia ya ushindi.
Mungu Ameongoza kila enzi kwa njia ambayo mwanadamu hawezi kuwazia. Hata katika enzi ya Roho Mtakatifu, tunapoamini kikamilifu maneno ya Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama, “Okoa ulimwengu,” tutatimiza misheni ya jeshi la mbinguni, ambayo ni kukamilisha injili ya ufalme.
Vumilia taabu pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu. Hakuna askari yeyote ambaye akiwa vitani hujishughulisha na mambo ya kawaida ya maisha haya kwa sababu nia yake ni kumpendeza yule aliyemwandika awe askari. 2 Timotheo 2:3–4
Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kwa sababu hii, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.” Mathayo 28:18–20
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha