Kama vile Koreshi, mfalme wa Uajemi, alivyogundua unabii kumhusu yeye katika Biblia na akaguswa sana kiasi kwamba akawaweka huru Waisraeli kutoka utumwani na kulijenga hekalu huko Yerusalemu, vivyo hivyo lazima tuamini unabii ulioandikwa katika Biblia. Tukiwa tumejawa na furaha ya kina kama Koreshi, lazima tuhubiri injili ambayo Mungu Ametuamuru kwa mioyo yetu yote na kwa roho zetu zote.
Kama Yesu Alivyofundisha kupitia Mfano wa Mafungu Kumi ya Fedha, Ameahidi mustakabali mtukufu kwa wale wanaoliheshimu neno la Mungu: watatawala pamoja na Mungu milele na milele, wakifurahia utukufu wa milele katika ufalme wa mbinguni—mahali ambapo mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu.
Kisha nikaona “mbingu mpya na nchi mpya”, kwa maana mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapakuwa na bahari tena. . . . Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” Ufunuo 21:1–4
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha