Wakati wa kutoka kwa Waisraeli, maafa yaliipata Misri yote, lakini maafa hayakuja juu ya Waisraeli. Hii ilikuwa tofauti hasa kati ya mahali penye agano la Mungu na mahali pasipo na agano hilo. Mungu Ametoa ahadi kuu kwamba popote amri Yake—Pasaka ya agano jipya—inapoadhimishwa, watu Wake watabarikiwa wanapoingia na watabarikiwa wanapotoka, naye Atawaweka juu juu ya mataifa yote duniani.
Manabii Isaya, Sefania, na Petro wanashuhudia kwamba maafa makubwa ya moto yatakuja juu ya dunia hii kwa sababu ulimwengu haushiki agano jipya, ambalo linajumuisha siku ya Sabato ya Mungu na Pasaka. Biblia inashuhudia kwamba ni kwa kulishika agano la Mungu tu wanadamu wanaweza kuwa watoto wa Baba Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama na kupokea ulinzi wa Mungu dhidi ya maafa yote.
Kama ukimtii Bwana Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, Bwana Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia. Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtii Bwana Mungu wako: . . . Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo. Kumbukumbu la Torati 28:1–6
“Utakapowaambia watu hawa mambo haya yote na wakakuuliza, ‘Kwa nini BWANA Ameamuru maafa makubwa kama haya dhidi yetu? Tumefanya kosa gani? Tumetenda dhambi gani dhidi ya BWANA, Mungu wetu?’ Basi waambie, ‘Ni kwa sababu baba zenu waliniacha mimi, wakafuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu. Waliniacha mimi na hawakuishika sheria yangu,’ ” Yeremia 16:10–11
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha