Kwa kuwa vitabu 66 vya Biblia vina njia ya kumwendea Mwokozi pamoja na hekima ya kupambanua kati ya ukweli na uongo, Mungu Anatuonya tusiongeze wala tusipunguze chochote kutoka kwenye Biblia, bali tuifuate tu kulingana na maneno ya Mungu. Miaka elfu mbili iliyopita, Yesu peke Yake Alipaza sauti na kusema, “Njooni kwangu kupokea maji ya uzima,” ila Yeye Mwenyewe Ametufundisha kwamba sasa ni lazima tuje kwa Roho na Bibi arusi ili kuyapokea maji ya uzima ili kuwa na uzima wa milele.
Isaya alitabiri kwamba Mungu Atawaongoza watoto Wake hadi kwenye chemchemi ya maji yaliyo hai, na Mungu Ahnsahnghong, ambaye ndiye Roho Mtakatifu, Aliyetimiza unabii wote wa Biblia, Amewaongoza wanadamu kwa Yerusalemu, Mama wa Mbinguni, ambaye ndiye Bibi arusi wa Roho Mtakatifu na chanzo cha maji ya uzima.
Roho na bibi arusi wanasema, “Njoo!” Naye asikiaye na aseme, “Njoo!” Yeyote mwenye kiu na aje, na kila anayetaka na anywe maji ya uzima bure. Ufunuo 22:17
Hili ndilo asemalo BWANA: “Wakati wangu uliokubalika nitakujibu, nami katika siku ya wokovu nitakusaidia; . . . Yeye mwenye huruma juu yao atawaonyesha njia, na kuwaongoza kando ya chemchemi za maji.” Isaya 49:8–10
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha