Watoto wa Mungu wanapokuwa chumvi na nuru ya ulimwengu kulingana na mafundisho ya Mungu, wakionyesha utukufu wa Mungu kupitia matendo yao mema, na kuwaongoza wanadamu kwa Mungu kwa ukweli wa agano jipya, Mungu Atapendezwa na kuwapa baraka tele siku watakaposimama mbele Zake.
Ikiwa tumempokea Kristo Ahnsahnghong na Yerusalemu Mama wa Mbinguni katika enzi ya Roho Mtakatifu, kuanzia sasa, lazima tuache mazoea mabaya tuliyojifunza kutoka ulimwenguni na kuvaa utu mpya kama Wakristo. Ulimwengu huu unapozidi kupoteza utauwa wake na kuwa mpotovu na mwovu, lazima tutambue kwamba siku ya hukumu ya Mungu imekaribia, kama ilivyokuwa katika siku za Noa na Loti, na tuishi maisha ya utauwa zaidi.
Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana. Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kujaribu ili kuthibitisha mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza na kamilifu machoni pake. Warumi 12:1–2
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha